Wasanii Nadia Mukami na Arrow Boy Waweke Wazi Penzi Lao

Publish date: 2024-08-30

Mafisi wanapitia hali ngumu baada ya Nadia Mukami kufichua kuwa yeye ni mali safi ya msanii Arrow Bow.

Kupitia video kwenye mtandao, wawili hao walisema sasa wamechoka kuficha penzi lao na wamesema liwe liwalo.

Nadia amekuwa matamanio ya wengi kutoka na uzuri wake na sauti nyororo ambayo amekuwa akiwapapasa nayo kwenye miziki.

Nadia alisema miaka imesonga pakubwa na sasa ni wakati shamba lake lipate mazao ili maisha kusonga mbele

"Ni wakati watu waamini kwani unajua saa hii miaka inasonga sana. Nazeeka, niko miaka 25 saa hii na ninahitaji kupanga maisha na mtu," Nadia alisema kwenye video hiyo.

Alisema baadhi ya marafiki wake wamekuwa wakizua maswali kuhusu uhusiano huo na akawataka wamwache aishi atakavyo.

Pia soma

Moto Gikomba: Wafanyabiashara Katika Soko la Gikomba Wapata Hasara

"Kuna vitu huwezi badilisha kuhusu watu. Ni vile mimi niliamua, na ilifika mahali ikawa ni ngumu kwetu kuendelea kuficha penzi hili," alisema.

Kulingana na msanii huyo, walikuwa wanakutana kwenye vikao ambapo walijifanya hawajuani licha ya kuwa walilala pamoja.

"Saa hizo tumelala katika nyumba moja, na tunajifanya hatujuani," alisema Nadia.

Wawili hao walisema penzi liliota wakati walianza kufanya muziki pamoja na sasa limewaka moto.

Urafiki wa wawili hao ulionekana wazi wakati wa wimbo wao maarufu wa Radio Love ingawa Arrow alisema moto ulianza kuwaka mapema.

Wanamtandao walisema ni wazi kwenye video hiyo kuwa Nadia anapepetwa na penzi la ndume huyo mwenye sifa za kunengua kiuno wakati wa mziki.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ39zfJZmrpqrkaO2qnnNmpuimV2iwqytzKJkp5ldlr%2Bzu9ZmmaixXayuuLHKnmSwmaqeerGxzbOgZqSRpHupwMyl